Maamuma ambaye anatakiwa kusujudu sijda ya kusahau

Swali: Anasujudu sijda ya kusahau ambaye amejiunga na imamu kwa kuchelewa? Lini anafanya hivo? Je, maamuma analazimika kusujudu sijda ya kusahau akisahau?

Jibu: Maamuma halazimiki kusujudu sijda ya kusahau akisahau. Ni lazima kwake kumfuata imamu wake akiwa amejiunga pamoja naye kuanzia mwanzoni mwa swalah. Kuhusu ambaye amejiunga hali ya kuchelewa anasujudu sijda ya kusahau akisahau nyuma ya imamu wake au katika yale aliyokosea pindi alipokuwa anaswali mwenyewe baada ya kukamilisha swalah kwa mujibu wa upambanuzi uliotangulia katika kujibu maswali mawili yaliyotangulia.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Majmuu´-ul-Fataawaa (11/268)
  • Imechapishwa: 31/10/2021