Swali: Ni ipi tofauti kati ya waislamu na Ahmadiyyuun/Qaadiyaaniyyuun?

Jibu: Tofauti kati yao ni kuwa waislamu ni wale wanaomuabudu Allaah Pekee na wanamfuata Mtume Wake Muhammad (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam). Vilevile wanaamini kuwa yeye ndiye Mtume wa mwisho na hakuna Nabii mwingine baada yake.

Ama kuhusu Ahmadiyyuun ambao ndio wafuasi Mirzaa Ghulaam Ahmad ni makafiri. Sio waislamu. Wanadai kuwa Mirzaa Ghulaam Ahmad ni Nabii baada Muhammad (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam). Mwenye kuamini imani hii ni kafiri kwa makubaliano ya wanachuoni wote wa waislamu. Allaah (Subhaanah) anasema:

مَّا كَانَ مُحَمَّدٌ أَبَا أَحَدٍ مِّن رِّجَالِكُمْ وَلَـٰكِن رَّسُولَ اللَّـهِ وَخَاتَمَ النَّبِيِّينَ

“Hakuwa Muhammad baba wa mmoja yeyote miongoni mwa wanaume wenu, lakini ni Mtume wa Allaah na ni mwisho wa Manabii.” (33:40)

Imesihi kutoka kwa Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) ya kwamba amesema:

“Mimi ndio Nabii wa mwisho. Hivyo basi hakuna Nabii baada yangu.”

  • Mhusika: al-Lajnah ad-Daaimah
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Fataawaa al-Lajnah ad-Daaimah (2/221-222)
  • Imechapishwa: 23/08/2020