Kukubaliana kwa wanachuoni juu ya ukafiri wa Qaadiyaaniyyah

Swali: Ninatarajia kutubainishia hukumu ya Uislamu juu ya kundi la Qaadiyaaniyyah na Mtume wao wa uongo Ghulaam Ahmad al-Qaadiyaaniy. Vilevile tunaomba kututumia kitabu chochote kinachozungumzia kuhusu kundi hili kwa vile mimi nina hamu ya kulisoma.

Jibu: Utume umekhitimishwa kwa Mtume wetu Muhammad (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam). Hivyo hakuna Mtume mwingine baada yake. Hilo limethibiti katika Qur-aan na Sunnah. Mwenye kudai utume baada ya hapo ni mwongo. Miongoni mwa watu hao ni Ghulaam Ahmad al-Qaadiyaaniy. Kudai kwake utume ni uongo. Wafuasi wake waliodai kwamba ni ukweli ni madai ya uongo.

Kikao cha baraza la wanachuoni wakubwa Saudi Arabia wamethibitisha kuwa Qaadiyaaniyyah ni kundi la kikafiri kwa ajili ya hilo [kudai kwao utume].

  • Mhusika: al-Lajnah ad-Daaimah
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Fataawaa al-Lajnah ad-Daaimah (221/02)
  • Imechapishwa: 23/08/2020