Swali: Wanadai baadhi ya watu kuwa Salafiyyah ni kama makundi mengine yote yalioko leo na hukumu yake ni kama hukumu ya makundi mengine yote. Wasemaje kuhusiana na madai haya?

Jibu: Hili ni kama tulivyosema. Kundi la Salafiyyah ndio kundi lililo katika haki. Nalo ndio wajibu kujinasibisha kwalo na kufanya kazi nalo. Makundi mengine yote hayazingatiwe kuwa ni makundi ya Da´wah. Kwa kuwa yanakwenda kinyume. Vipi tutafuata kundi liendalo kinyume na kundi la Ahl-us-Sunnah na uongofu wa Salaf-us-Swaalih? Kundi liendalo kinyume na Salafiyyah ni kundi linakhalifu mfumo wa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam). Linakhalifu aliokuwemo Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) na Maswahabah wake. Kauli yake kuwa kundi la Salafiyyah ni kama makundi mengine yote ya Kiislamu, hili ni kosa. Kundi la Salafiyyah ndio kundi pekee ambalo ni wajibu kulifuata na kupita katika mfumo wake na kujiingiza humo na kupigana nalo Jihaad. Na kundi lingine haijuzu kwa muislamu kujiingiza humo, kwa kuwa linakhalifu. Na je, ataridhia muislamu kujiingiza kwa wanaokhalifu? Muislamu haridhii hili. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) anasema:

“Lazimianeni na Sunnah zangu na Sunnah za makhaliyfah wangu waongofu na wenye kuongoza baada yangu.”

Vilevile Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Kundi lililookoka ni lile lilioko kwa yale niliyomo leo mimi na Maswahabah wangu.”

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: http://www.salafi.ws/@TASGELAT/fo-30.mp3
  • Imechapishwa: 09/04/2022