Tofauti ya mwanachuoni na anayejifanya mwanachuoni

Swali: Ni vipi mwanafunzi katika wakati huu ambapo fitina imekithiri ataweza kupambanua baina ya mwanachuoni na anayejifanya kuwa ni mwanachuoni ili aweze kuchukua elimu kutoka kwa wale wenye kustahiki?

Jibu: Wanachuoni wanajulikana, hawakufichikana. Watu wanajua ni wepi. Wanarejea kwao na kuwaiga. Mwanachuoni anaonekana, hafichikani. Mwenye kujifanya ni mwanachuoni pia huonekana. Ambaye hakusoma kwa wanachuoni ni mwenye kujifanya mwanachuoni. Ambaye anasoma vitabu mwenyewe anajifanya kuwa ni mwanachuoni. Hawezi kuwa mwanachuoni midhali waalimu zake hawajulikani. Ni kina nani waalimu zake? Elimu yake ameitoa wapi? Elimu ni kama nasabu. Mtu asiyekuwa na waalimu ni kama yatima mwenye kuokotwa. Hili sio suala sahali. Elimu sio kitu sahali. Ni lazima kwa elimu ichukuliwe kutoka kwa wanachuoni wenye kujulikana, wenye kushikamana nayo na kuitendea kazi.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Ighaathat-il-Lahfaan (35) http://www.alfawzan.af.org.sa/sites/default/files/ighasah%20%20-%2017-%2010-1436.mp3
  • Imechapishwa: 12/02/2017