Da´wah Haihitajii Facebook, Instagram Na Twitter

Swali: Umezipa kisogo njia za mawasiliano ya leo kama mfano wa Twitter. Ina maana ya kwamba mwanafunzi aziepuke kikamilifu au azitumie katika mambo ya manufaa kama Da´wah na masomo?

Jibu: Lililo bora na salama zaidi kwake ni yeye kujiepusha nazo. Kulingania katika dini ya Allaah ni jambo lina njia zake zilizowekwa katika Shari´ah kabla ya kuzuka mambo haya. Lingania katika dini ya Allaah kwa kuita katika Qur-aan na Sunnah, wafunze watu elimu yenye manufaa na wabainishie hukumu za Kishari´ah, waamrishe mema na kuwakataza maovu kwa hekima, maneno mazuri, kutoka wende katika Jihaad na kulingania. Hakuna haja ya mambo haya. Ni mambo yanashughulisha. Unaweza kuona kitu kama ni kizuri ukatumbukia ndani yake. Salama zaidi ni kujiepusha nazo. Hauna haja nazo na himdi zote ni za Allaah.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Ighaathat-il-Lahfaan (35) http://www.alfawzan.af.org.sa/sites/default/files/ighasah%20%20-%2017-%2010-1436.mp3
  • Imechapishwa: 12/02/2017