Swali: Katika mji wangu hakuna wanachuoni. Ni ipi njia sahihi ya kutafuta elimu sahihi? Nataka kuhama kwenda Saudi Arabia na ar-Riyaadh kutafuta elimu, lakini baba yangu hataki. Nifanye nini?

Jibu: Allaah (Jalla wa ´Alaa) amesema:

وَمَا كَانَ الْمُؤْمِنُونَ لِيَنفِرُوا كَافَّةً ۚ فَلَوْلَا نَفَرَ مِن كُلِّ فِرْقَةٍ مِّنْهُمْ طَائِفَةٌ لِّيَتَفَقَّهُوا فِي الدِّينِ وَلِيُنذِرُوا قَوْمَهُمْ إِذَا رَجَعُوا إِلَيْهِمْ لَعَلَّهُمْ يَحْذَرُونَ

“Na haiwapasi waumini watoke wote pamoja kwenda. Basi kwanini lisitoke katika kila kundi miongoni mwao kundi wakajifunza dini ili waonye watu wao watakaporejea kwao ili wapate kutahadhari.” (09:122)

Ikiwa katika nchi yako hakuna wanachuoni safiri uwaendee. Huhitajii kukaa kwao maisha yote. Ni sawa kuwa huko mwezi mmoja, nusu ya mwezi, baadhi ya siku na kurejea. Safiri uwaendee. Leo njia za safiri imekuwa ni rahisi. Leo kusafiri imekuwa ni sahali kuliko hapo kabla. Hapo kabla watu walikuwa wakienda masafa ya mbali kwa miguu yao kuwaendea wanachuoni. Imaam Ahmad alisafiri kwenda Yemen[1] kwa ajili ya kusoma chini ya Imaam ´Abdur-Razzaaq as-Swan´aaniy. Alisafiri. Hapo kabla watu walikuwa wakisafiri kwa miguu yao. Walikuwa ni wageni katika miji mingine kwa ajili tu ya kutafuta elimu. Walikuwa hawana kitu. Inatakiwa siku zote kusafiri kwenda kwa wanachuoni. Leo usafiri imekuwa ni rahisi. Leo kutokamana na umbio wa usafiri unaweza kusafiri mwishoni mwa dunia na ukarudi nyumbani katika siku hiyo hiyo.

[1] Bagdad-Sanaa, 2675 km, 538 h.

Tazama https://www.google.se/maps/dir/Sanaa,+Amanat+Al+Asimah,+Yemen/Bagdad,+Irak/@24.0696778,35.7608778,5z/data=!3m1!4b1!4m14!4m13!1m5!1m1!1s0x1603dbd54684f731:0xa46b957a1482ac73!2m2!1d44.1910066!2d15.3694451!1m5!1m1!1s0x15577f67a0a74193:0x9deda9d2a3b16f2c!2m2!1d44.422!2d33.325!3e2?hl=sv

 

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Ighaathat-il-Lahfaan (35) http://www.alfawzan.af.org.sa/sites/default/files/ighasah%20%20-%2017-%2010-1436.mp3
  • Imechapishwa: 12/02/2017