Tofauti ya moyo ulio hai na moyo mgonjwa

Ukiona kila unaposoma Qur-aan imani inaongezeka kwenye moyo wako, basi ujue kuwa hii ni alama ya mafanikio. Kinyume chake ukiona unasoma Qur-aan na wala huathiriki nayo, basi itibu nafsi yako. Simaanishi uende kuitibu kwa madawa ya hospitali, bali irekebisheni nafsi yako. Hakika moyo ikiwa haunufaiki kwa Qur-aan, basi huyo ni moyo ulio mgonjwa.

Ndugu yangu! Wewe mwenyewe ndiye tabibu wa moyo wako na huhitajii kwenda kwa watu. Soma Qur-aan na pale utapoona unaathirika nayo kwa kuiamini na kuisadikisha na kuitendea kazi, basi nakupa bishara njema. Hakika wewe ni muumini. Ikiwa ni kinyume chake, basi unalazimika kuitibu nafsi yako. Itibu nafsi yako kabla hayajakujia mauti yasiyokuwa na uhai baada yake. Huku ndio kufa kwa moyo. Ama kuhusiana na mauti ya kiwiliwili baada yake yana uhai. Mauti haya baada yake kuna kufufuliwa, malipo na kuhesabiwa.

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Riyaadh-is-Swaalihiyn (01/545)
  • Imechapishwa: 16/07/2023