Sababu ya wanawake kuwa wengi kuliko wanaume

Swali: Ni kwa nini katika zama za mwisho wanawake watakuwa wengi zaidi kuliko wanaume?

Jibu: Ni kwa sababu – na Allaah ndiye mjuzi zaidi – ni kwa sababu ya vita vingi na majanga. Wanaume watauliwa na wanawake watakuwa wengi kiasi cha kwamba itafikia mwanaume mmoja kuwa na wanawake arobaini na tano. Wasimamizi watakuwa wachache na wanawake watakuwa wengi. Hilo – na Allaah ndiye mjuzi zaidi – ni kwa sababu ya vita vitavyotokea katika miji mingi mara kwa mara.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/22671/ما-سبب-كثرة-النساء-عن-الرجال-اخر-الزمان
  • Imechapishwa: 16/07/2023