Tofauti ya maimamu wa Salaf na wajinga leo juu ya Jarh wa Ta´diyl

Ibn-ul-Qayyim (Rahimahu Allaah) amesema:

“Muhammad bin Jariyr amesema: Ibn Humayd ametuhadithia: Ibraahiym bin al-Mukhtaar ametuhadithia, kutoka kwa Ibn Jurayj, kutoka kwa ´Atwaa´, kutoka kwa Ka´ba bin ´Ujrah, kutoka kwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam).”

Hapa kuna Muhammad bin Humayd ar-Raaziy ambaye wanachuoni wa Hadiyth wamemtia dosari. Imaam Ahmad amemtakasa na wengine wakamkosoa na kumdhoofisha na wakapitiliza katika kumdhoofisha. Miongoni mwa ambao wamemdhoofisha ni Ibn Khuzaymah (Rahimahu Allaah). Alipoambiwa kuwa Imaam Ahmad amesema kuwa ni mwadilifu au amemtakasa akasema:

“Lau Ahmad angelimjua jinsi tunavyomjua basi asingemtakasa.”

Huu ndio mfumo ambao wanapita juu yake Ahl-us-Sunnah wal-Jamaa´ah na maimamu wa Hadiyth. Nao ni kwamba mwenye kujua ni hoja juu ya yule asiyejua na kwamba kujeruhi, Jarh kunatangulia kabla ya kusifu, Ta´diyl. Hakuna upungufu katika hili kwa imamu yoyote awae. Imamu fulani anapomsifu mtu kisha akaja imamu mwingine mfano wake au ambaye yuko chini kuliko yeye na akawa amethibitisha kwa hoja na dalili ambapo akamsema vibaya mtu huyu ambaye amesifiwa na imamu yule. Hakuna mapungufu ndani yake na wala hili halichukuliwi kwa ubaya. Wanazunguka kwa hoja na dalili. Wanachokusudia ni haki na Uso wa Allaah (´Azza wa Jall). Hawajali kwa ajili ya Allaah lawama za wenye kulaumu. Hawakusema kuwa mtu huyu amesifiwa na Ahmad, ash-Shaafi´iy au mtu mwingine. Hawasemi ni kwa nini amemjeruhi. Hapana, hawasemi maneno haya. Wanazumgumza kwa haki na hawaonelei tatizo juu ya hilo.

Lakini leo tuko katika zama za giza na ujinga mkubwa ambapo Ahl-ul-Bid´ah wal-Ahwaa´ wameingiza katika mfumo wa Ahl-us-Sunnah wal-Jamaa´ah. Imaam Ahmad ndio Imaam wa Ahl-us-Sunnah. Je, kuna yeyote aliyesema kuwa Ibn Waarah, al-Bukhaariy, Abu Zur´ah, Ibn Haatim, Ibn Khuzaymah na wengineo ambao wamemkosoa Muhammad bin Humayd ya kwamba kufanya hivi ni kumwangusha Ahmad na kumkhalifu? Ikiwa kuna ambaye amesifiwa na Ahmad na wengine wao ndio wako na hoja, basi utaona wanaume wa Ahmad na ash-Shaafi´iy wanakubali jeruhi ya huyu mwenye hoja. Kadhalika wafuasi wa ash-Shaafi´iy wakimsifu mtu mfano wa Muhammad bin Ibraahiym bin Abiy Yahyaa na wengine wakamjeruhi, wanapokea jeruhi hii na hawasemi kuwa Imaam wetu [ash-Shaafi´iy] amemsifu.

Ndugu! Kuweni ni wenye kulelewa juu ya mfumo huu uliobarikiwa mzuri. Ni wajibu kuachana na ushabiki kwa mtu yeyote na vyovyote atavyokuwa. Inatakiwa kuwa na ushabiki kwa Muhammad (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) peke yake. Yeye peke yake ndiye ambaye hakosolewi na haikubaliki kwa yeyote kutofautiana naye. Kadhalika Maswahabah wa Muhammad (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) ni wenye kwenda na haki popote inapokuwa. Isipokuwa tu pale wanapotofautiana kunachukuliwa kauli ya yule ambaye ina nguvu zaidi kuliko mwingine. Mbali na hawa wengine wote kauli zao zinachukuliwa na kuachwa (Radhiya Allaahu ´anhum) na (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam).

  • Mhusika: ´Allaamah Rabiy´ bin Haadiy al-Madkhaliy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-Bayaan wa al-Idhwaah li ´Aqiydah Ahl-is-Sunnah wal-Jamaa´ah fiy Ru´yati Allaahi yaum al-Qiyaamah, uk. 37-39
  • Imechapishwa: 27/08/2020