Asad as-Sunnah alikuwa ni mmoja katika Mujaahiduun ambaye alikuwa anajulikana kwa uadilifu na kuitendea kazi Sunnah na kuwaponda Ahl-ul-Bid´ah. Asad bin Muusa al-Umawiy (Rahimahu Allaah) – ambaye alikuwa ni mmoja katika wanachuoni na maimamu wa Hadiyth na Ahl-us-Sunnah – akamwandikia Asad as-Sunnah huyu – ambaye alikuwa ni mmoja katika Mujaahiduun wakubwa na mwenye kupambana na Ahl-ul-Bid´ah wadh-Dhwalaal – kitabu kikubwa akimshukuru kuwaponda kwake Ahl-ul-Bid´ah wadh-Dhwalaal. Ahl-us-Sunnah walikuwa namna hii. Walikuwa wanafurahishwa Ahl-ul-Ahwaa´ wakipondwa na wanamshukuru mwenye kufanya kazi hiyo. Akifanya ukali basi ukali wake huu unakuwa ni wenye kusifiwa.

Ama katika zama zetu hii leo kuwaponda Ahl-ul-Bid´ah kwa masikitiko makubwa wanaonelea kuwa ni katika mambo yenye kulaumiwa.

Leo wanakuhukumu kwa Sayyid Qutwub na wanakabiliana na wewe juu yake kwa nini unamkosoa! Mwache amfanyie maskhara Mtume wa Allaah Muusa, mwache awatukane Maswahabah na khaswa ´Uthmaan (Radhiya Allaahu ´anh). Ni Uislamu upi ambao wanataka kueneza ikiwa wanaghadhibishwa kwa ajili ya Ahl-ul-Bid´ah wakubwa na wanawapiga vita Ahl-us-Sunnah kwa ajili yao.

  • Mhusika: ´Allaamah Rabiy´ bin Haadiy al-Madkhaliy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-Bayaan wa al-Idhwaah li ´Aqiydah Ahl-is-Sunnah wal-Jamaa´ah fiy Ru´yati Allaahi yaum al-Qiyaamah, uk. 43-44
  • Imechapishwa: 27/08/2020