Tofauti ya kumkufurisha mtu na kitendo au maneno yake

Swali: Mwenye kusema au kufanya kitu cha Shirki mtu aseme kuwa ni kafiri? Ni ipi dhwaabit ya hilo?

Jibu: Mtu aseme kuwa amefanya kufuru. Ikiwa ni Muislamu na akafanya au akasema kitu cha Shirki, mtu aseme kuwa amefanya tendo au maneno ya kufuru. Apewe kile anachostahiki. Ama kuhusu mtu kwa dhati yake, asihukumiwe kufuru mpaka kwanza asimamishiwe hoja, abainishiwe na aulizwe kwa kile alichokitamka au alichokifanya. Baada ya kusimamishiwa hoja na akawa ni mwenye kuendelea na Shirki, hapo ndio afanyiwe Takfiyr. Ama kabla ya hapo, maneno au maneno atakachofanya kipewe haki inayostahiki kwa kusema ´maneno haya ni ya kufuru” au “kitendo hichi ni cha kufuru`. Ama kuhusu mtu kwa dhati yake hatujui haki yake na hivyo hatuwezi kumkufurisha mpaka tumuulize kwanza na kumbainishia kwa kumwambia ´ewe fulani! Maneno au kitendo hichi ni kufuru`. Baadhi ya watu unapombainishia kitendo hichi ni cha kufuru anajirudi na kumuomba Allaah msamaha. Akijirudi, Alhamdulillaah, na akiendelea na kufuru baada ya kumsimamishia hoja hapo ndio anahukumiwa Shirki.

  • Mhusika: ´Allaamah ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah ar-Raajhiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: http://subulsalam.com/play.php?catsmktba=11649
  • Imechapishwa: 17/11/2014