Tofauti ya kufanya Tawassul na kuomba kwa sifa ya Allaah

Swali: “Ee Uliye hai, Mwenye kuyasimamia mambo yote, ninaomba uokozi kwa huruma  Yako.” Vipi nitaoanisha kati ya hili na makatazo ya kuomba sifa?

Jibu: Huku sio kuomba sifa. Huku ni kufanya Tawassul kwa sifa. Ni kama mfano wa kuomba:

“Ninakuomba kwa majina na sifa Zako.”

Kwa (biy) huku ni kufanya Tawassul kwa majina na sifa za Allaah. Huruma ni moja katika sifa za Allaah (Subhaanah). Hivyo ni kutawassul kwa sifa. Sio kuomba du´aa kwa sifa. Hakusema:

“Ee huruma ya Allaah.”

Hakuomba sifa ya huruma ya Allaah.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Qaa´idah Jaliylah fiyt-Tawassul wal-Wasiylah (22) http://www.alfawzan.af.org.sa/node/2134
  • Imechapishwa: 10/07/2020