Tofauti ya ghera waliokuwa nayo Maswahabah na sisi

´Abdullaah bin ´Umar alikuwa akimweleza mtoto wake na kusema:

“Msiwazuie wajakazi wa Allaah na misikiti ya Allaah.”

Alikuwa anaelezea juu ya idhini ya Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) wanapoomba idhini wapewe ili waweze kuswali Misikitini. Mtoto wake akasema:

“Ninaapa kwa Allaah, tutawazuia.”

Yaani alikuwa na ghera. Ibn ´Umar akamwambia:

“Ninakueleza aliyosema Mtume wa Allaah na wewe unasema kuwa utawazuia?” Akamkasirikia na kumtukana vibaya sana. Katika upokezi mwingine ambao sikumbuki usahihi wake kwamba alimsusa.

Kadhalika ´Abdullaah bin Mughaffal alikuwa akimweleza mtoto wa kaka yake alikuwa kwake na akasema:

“Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amekataza kutupa jiwe.”

Yule mtoto akawa ametupa jiwe. Akasema – yaani ´Abdullaah bin Mughaffal:

“Ninakueleza kuwa Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amekataza kutupa jiwe na wewe unatupa? Sintokusemeza.” Katika upokezi wa Muslim imekuja: “Sintokusemeza kamwe.”

Leo mtu anaenda kinyume na Kitabu cha Allaah na Sunnah za Mtume Wake kwa Bid´ah, upotevu na upindaji, yanaonekana kuwa ni mambo ya kawaida, usipingane naye akakimbia, tuache sote tuwe ndugu na kadhalika, tunasahihisha na hatujeruhi, kanuni: tushirikiane kwa yale tunayoafikiana na tupeane udhuru kwa yale tunayotofautiana, kuna Rawaafidhw, Suufiyyah, waabudu makaburi, sote tuwe ndugu! Iko wapi ghera juu ya Sunnah ya Mtume wa Allaah na juu ya dini ya Allaah? Huyu Raafidhwiy anaenda kinyume na Qur-aan kuanzia mwanzo wake mpaka mwisho wake, huyu Suufiy ana upotevu, shirki na Bid´ah, anaenda kinyume na Qur-aan na Sunnah pamoja na hivyo humkemei!

Hawa Maswahabah watatu wa Mtume wa Allaah ambao tumewataja na wengineo, ´Umar ana ghera kuliko wao, ninaapa kwa Allaah kwamba ´Umar bin al-Khattwaab ana ghera kuliko wao, ghera ya watu hawa iko katika makosa! Je, wewe uko katika mfumo sahihi kuliko mfumo wa watu hawa?!

  • Mhusika: ´Allaamah Rabiy´ bin Haadiy al-Madkhaliy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: adh-Dhariy´ah ilaa Bayaan Maqaaswid Kitaab-ish-Sharï´ah (1/562-563)
  • Imechapishwa: 26/08/2020