Tofauti ya “Akitaka allaah” na “Akipenda Allaah”

Ahl-us-Sunnah wal-Jamaa´ah wameyakusanya maandiko na wakagawa matakwa katika vigawanyo viwili (matakwa ya Kishari´ah na ya kilimwengu). Hawakufanya hivo kujitolea kwao wenyewe, bali wameyatoa kwenye maandiko.

Matakwa ya kilimwengu ni yale yenye kutajwa na waislamu kwenye msemo wao: “Anayoyataka Allaah huwa, Asiyoyataka hayawi”.

Kuhusu matakwa ya kidini na Kishari´ah, ni yale yenye kutajwa na watu: “Huyu anafanya mambo Asiyoyataka Allaah” wakiwa na maana ya kwamba anafanya mambo Asiyoyapenda Allaah. Kwa ajili hii lau mtu atasema: “Nitafanya kitu kadhaa Allaah akitaka [in shaa Allaah]” kisha asikifanye, hana juu yake kitu. Haijalishi kitu hata kama hicho alichotaka kufanya ilikuwa ni kitu cha wajibu au cha Sunnah. Akisema: “Wallaahi nitaswali Dhuhaa Allaah akitaka” na kisha asiswali, hana juu yake kitu kwa kuwa amefungamanisha na matakwa [ya Allaah ambayo ni ya kilimwengu]. Lakini akisema: “Nitaswali Dhuhaa Allaah akipenda [in ahabba Allaah]” na kisha asiswali, juu yake ni lazima kutoa kafara ya yamini kwa kuwa Allaah anapenda aswali Dhuhaa.

  • Mhusika: ´Allaamah ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah ar-Raajhiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-Hidaayah ar-Rabbaaniyyah fiy Sharh al-´Aqiydah at-Twahaawiyyah (01/57)
  • Imechapishwa: 07/06/2020