Tofauti kati ya mazazi ya Mtume na wiki ya Ibn ´Abdil-Wahhaab

Swali: Ni ipi tofauti kati ya yale yanayoitwa ´wiki ya Shaykh Muhammad bin ´Abdil-Wahhaab (Rahimahu Allaah)` na kusherehekea mazazi ya Mtume kwa vile hili la kwanza linapingwa tofauti na lile la kwanza?

Jibu: Tofauti kati ya hayo mawili, kutokana na vile ninavyojua, ni kwa njia mbili:

Ya kwanza: Wiki ya Shaykh Muhammad bin ´Abdil-Wahhaab (Rahimahu Allaah) haikufanywa hali ya kujikurubisha kwa Allaah (´Azza wa Jall). Kilichokusudiwa ni kuondosha utata unaopatikana kwenye vifua vya baadhi ya watu dhidi ya mtu huyu na watu wanabainishiwa neema ya Allaah juu ya mtu huyu.

Ya pili: Wiki ya Shaykh Muhammad bin ´Abdil-Wahhaab (Rahimahu Allaah) si yenye kukariri na yenye kujirudi kama zinavyojirudi sikukuu zengine. Ni jambo linalobainishwa kwa watu na kunaadikwa yanayoandikwa na yanapata kubainika kwa mtu huyu yale ambayo hayakuwa ni yenye kutambulika hapo kabla kwa watu wengi. Baada ya hapo mambo yanakwisha.

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Majmuu´-ul-Fataawaa (02/300)
  • Imechapishwa: 10/07/2017