Toa swadaqah pesa, na sio heshima yako

Swali: Je, inafaa kwangu kumuomba Allaah (Ta´ala) kwa kusema:

“Ee Allaah! Nimeitoa swadaqah heshima yangu kwa watu.”?

Jibu: Hapana, muombe Allaah akusalimishe. Unaitoa heshima yako swadaqah? Toa swadaqah pesa. Kama unataka malipo toa swadaqah pesa. Kuhusu heshima yako usiitoe swadaqah na wala usimruhusu yeyote akuseme vibaya.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Ta´liyqaat ´alaa Risaalah wujuub-il-´Amr bil-Ma´ruuf wan-Nahiy ´an al-Munkar (05)
  • Imechapishwa: 22/02/2024