Panga wakati wa kufanya kazi na kutafuta elimu

Swali: Unawanasihi nini wanafunzi ambao wanajishughulisha na elimu na wanafanya mapungufu katika haki za nyumba zao na watoto wao na hawafanyi kazi kwa sababu eti ambaye kufanya kazi kutamshughulisha kutokana na kutafuta elimu hatojifunza?

Jibu: Sio sahihi. Unafanya mapungufu upande mmoja na unasimamia vizuri upande mwingine. Haifai. Kusanya kati ya yote mawili na wakati huohuo usimamie mahitaji ya watoto wako. Kutafuta elimu kuna wakati wake na kutafuta riziki na kufanya kazi kuna wakati wake mwingine. Yapange mambo yako.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Ta´liyqaat ´alaa Risaalah wujuub-il-´Amr bil-Ma´ruuf wan-Nahiy ´an al-Munkar (03)
  • Imechapishwa: 22/02/2024