Sio sharti kwa yule ambaye anaamrissha mema na kukemea maovu awe amekingwa na makosa. Sote tuna makosa na mapungufu. Lakini hata hivyo inatakiwa kutubia kwa Allaah (´Azza wa Jall) wakati wote na kumuogopa Allaah (´Azza wa Jall). Kwa hiyo tunaamrisha mema na kukataza maovu hata kama kutakuwa na mapungufu. Tusikusanye kati ya kuacha kuamrisha mema na kukataza maovu na mapungufu na hivyo tukawa tumekusanya kati ya makosa mawili makubwa. Baadhi ya watu wanasema kuwa hawaamrishi mema wala kukataza maovu kwa sababu eti wao wenyewe hawafanyi mambo hayo. Hapana. Kuamrisha mema na kukataza maovu hakudondoki kutoka kwako ingawa utayafanya. Ukiyafanya, tubia kwa Allaah. Mlango wa tawbah umefunguliwa. Haukufungwa kwako. Hata hivyo usiache wajibu wa kuamrisha mema na kukataza maovu na hivyo ukakusanya kati ya makosa mawili makubwa; kosa la dhambi unayofanya na kuacha wajibu wako.
- Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
- Mfasiri: Firqatunnajia.com
- Marejeo: Ta´liyqaat ´alaa Risaalah wujuub-il-´Amr bil-Ma´ruuf wan-Nahiy ´an al-Munkar (04)
- Imechapishwa: 21/02/2024
Sio sharti kwa yule ambaye anaamrissha mema na kukemea maovu awe amekingwa na makosa. Sote tuna makosa na mapungufu. Lakini hata hivyo inatakiwa kutubia kwa Allaah (´Azza wa Jall) wakati wote na kumuogopa Allaah (´Azza wa Jall). Kwa hiyo tunaamrisha mema na kukataza maovu hata kama kutakuwa na mapungufu. Tusikusanye kati ya kuacha kuamrisha mema na kukataza maovu na mapungufu na hivyo tukawa tumekusanya kati ya makosa mawili makubwa. Baadhi ya watu wanasema kuwa hawaamrishi mema wala kukataza maovu kwa sababu eti wao wenyewe hawafanyi mambo hayo. Hapana. Kuamrisha mema na kukataza maovu hakudondoki kutoka kwako ingawa utayafanya. Ukiyafanya, tubia kwa Allaah. Mlango wa tawbah umefunguliwa. Haukufungwa kwako. Hata hivyo usiache wajibu wa kuamrisha mema na kukataza maovu na hivyo ukakusanya kati ya makosa mawili makubwa; kosa la dhambi unayofanya na kuacha wajibu wako.
Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
Mfasiri: Firqatunnajia.com
Marejeo: Ta´liyqaat ´alaa Risaalah wujuub-il-´Amr bil-Ma´ruuf wan-Nahiy ´an al-Munkar (04)
Imechapishwa: 21/02/2024
https://firqatunnajia.com/si-sharti-ili-ulinganie-uwe-umekamilika/
Mshirikishe mwenzako:
- Click to share on Telegram (Opens in new window)
- Click to share on WhatsApp (Opens in new window)
- Click to print (Opens in new window)
- Click to email a link to a friend (Opens in new window)
- Click to share on Facebook (Opens in new window)
- Click to share on Twitter (Opens in new window)
- Click to share on Pocket (Opens in new window)