Swali: Ikiwa wanazuoni wamekinzana juu ya maovu fulani kati ya wanaojuzisha na wanaoharamisha. Je, ni lazima…

Jibu: Hutakiwi kutazama maono. Unachotakiwa kuzingatia ni dalili. Yule ambaye ameisibu dalili katika wenye kutofautiana ndiye ambaye yuko katika haki. Ambaye ameenda kinyume na dalili mwache. Hilo ndilo unatakiwa kutazama. Uko na mizani: Qur-aan na Sunnah:

فَإِن تَنَازَعْتُمْ فِي شَيْءٍ فَرُدُّوهُ إِلَى اللَّـهِ وَالرَّسُولِ إِن كُنتُمْ تُؤْمِنُونَ بِاللَّـهِ وَالْيَوْمِ الْآخِرِ ۚ ذَٰلِكَ خَيْرٌ وَأَحْسَنُ تَأْوِيلًا

”Mkizozana juu ya jambo, basi lirudisheni kwa Allaah na Mtume mkiwa mnamuamini Allaah na siku ya Mwisho. Hivyo ni bora na matokeo mazuri kabisa.”[1]

Hatubaki kwenye tofauti na kusema muda wa kuwa kuna tofauti basi tumwache kila mmoja afuate matamanio yake. Ikiwa kuna tofauti na dalili iko na moja kati ya makundi mawili, fuata dalili.

[1] 04:59

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Ta´liyqaat ´alaa Risaalah wujuub-il-´Amr bil-Ma´ruuf wan-Nahiy ´an al-Munkar (04)
  • Imechapishwa: 21/02/2024