Thawabu za Qur-aan na swawm siku ya ´Arafah au ´Aashuuraa´ kwenda kwa maiti

Swali: Je, inafaa kusoma Qur-aan, kufunga siku ya ´Arafah na siku ya ´Aashuuraa´ na kumpa thawabu zake yule maiti?

Jibu: Hapana, maiti hafungiwi swawm ya kujitolea wala kusoma kwa ajili yake. Hakuna katika Sunnah kinachofahamisha jambo hilo. Kutokana na ninavyojua hakuna katika Sunnah kinachojulisha kumpa maiti thawabu za kisomo cha Qur-aan, kumfungia, kumswalia. Lakini kama aliacha deni la funga anapaswa kufungiwa. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Yule anayekufa na anadaiwa swawm, basi atafungiwa na walii wake.”

Kutokana na ninavojua kumswalia au kumsomea Qur-aan ni mambo hayakuwekwa katika Shari´ah. Yaliyosuniwa ni kumtolea swadaqah, kumuombea du´aa, kumuhijia, kumfanyia ´umrah na kumlipia deni lake kama aliacha deni.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/15596/حكم-تثويب-قراءة-القران-وصيام-التطوع-للميت
  • Imechapishwa: 23/07/2023