Amekosa siku ya ´Aashuuraa´ kwa kusahau akafunga siku nyingine badala yake

Swali: Mimi ni mtu ninayefunga siku ya ´Arafah kila mwaka na pia ´Aashuuraa´. Hata hivyo mwaka uliyopita nilisahau siku ya ´Aashuuraa´ kwa sababu nilikula siku hiyo kwa kusahau kuwa ni siku ya ´Aashuuraa´. Lakini nilikamilisha swawm yangu na nikafunga siku ya tarehe kumi na moja. Je, kitendo changu hichi ni sahihi?

Jibu: ´Aashuuraa´ yote ni nzuri. Ukifunga zile siku utazojaaliwa ni vizuri. Tunataraji kuwa umepata thawabu ile siku iliyokupita kwa sababu ya kusahau. Uliiacha kwa kutokukusudia. Ulisahau. Ulipata thawabu – Allaah akitaka. Ni vizuri ulifunga siku ya tarehe kumi na moja. Kwa sababu siku ya kumi uliikosa kwa kusahau na hivyo unapata thawabu. Ni kama ambavo ungeacha kufunga kwa sababu ya ugonjwa kisha ukapona siku ya tarehe kumi na moja.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/15366/حكم-من-اعتاد-صيام-عاشوراء-ثم-فاته-صيامه-ناسيا
  • Imechapishwa: 23/07/2023