Swali: Thawabu za swadaqah yenye kuendelea zinasimama kwa kusimama sababu yake kwa mfano yakakauka ndani ya kisima? Aidha elimu ambayo watu wananufaika nayo zinasimama thawabu zake kwa kusimama sababu yake?

Jibu: Midhali watu wananufaika nayo basi thawabu ni zenye kubakia. Ikikatika basi thawabu pia zinasimama.

Swali: Thawabu haziendelei?

Jibu: Zinasimama kwa kusimama thawabu zake.

Swali: Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Anapofariki mwanadamu basi matendo yake yote hukatika isipokuwa vitu vitatu; swadaqah yenye kuendelea, elimu ambayo watu wananufaika kwayo au mtoto mwema anayemuombea du´aa.”

Je, swadaqah yenye kuendelea na elimu ambayo watu wananufaika kwayo vinalingana au hakuna tofauti kati ya hayo mawili?

Jibu: Allaah ndiye mjuzi zaidi. Muhimu anapata thawabu kwa Allaah.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/22974/هل-ينقطع-اجر-الصدقة-والعلم-بانقطاع-السبب
  • Imechapishwa: 23/09/2023