Swali 27: Mwezi ulipasuka lini?

Jibu: Mwezi ulipasuka baada ya safari ya usiku na ya kupandishwa usiku. Wakati washirikina walipomuomba (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) awaonyeshe ishara akawaonyesha mwezi ukiwa umegawanyika vipande viwili. Kipande kimoja kikiwa juu ya mlima wa Abu Qubays na kipande kingine nyuma yao. Akasema: ”Shuhudieni! Ambapo wakasema: ”Uchawi wenye kuendelea!”[1]

[1] al-Bukhaariy (3868) na (4864) na Muslim (2800).

  • Mhusika: ´Allaamah Haafidhw bin Ahmad al-Hakamiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Amaaliy fiys-Siyrah an-Nabawiyyah, uk. 100
  • Imechapishwa: 23/09/2023