Swali: Ni ipi nasaha yako kwa yule ambaye anasoma Qur-aan kidogo?

Jibu: Nasaha zetu asome Qur-aan kwa wingi. Qur-aan ni nyepesi. Jaalia wakati sawa ikiwa ni usiku au mchana usome kile ambacho itakuwa sahali kwako na udumu kufanya hivo. Kudumu juu ya jambo la kheri, hata kama jambo hilo litakuwa dogo, ndani yake kuna kheri kubwa. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Kitendo kinachopendwa sana na Allaah ni kile chenye kudumu hata kama kitakuwa kichache.”

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: http://www.alfawzan.af.org.sa/sites/default/files/liqo%20%20-%2021%20-%2008%20-%201435.mp3
  • Imechapishwa: 09/04/2015