Tazama matendo yake, na si yale anayofanya

Swali: Ni ipi hukumu ya mtu ambaye anadhihirisha baadhi ya mambo mbele ya umati wa watu na huku akidai kuwa ni karama?

Jibu: Kuna kidhibiti kilichotajwa na Allaah. Karama hazimpitikii isipokuwa yule aliye muumini na mchaji Allaah. Usiyatazame yale mambo anayofanya yasiyokuwa ya kawaida.

Yatazame matendo yake. Ikiwa matendo yake ni mema, basi yale anayofanya yanazingatiwa kuwa ni karama kutoka kwa Allaah. Na ikiwa matendo yake ni maovu, yanazingatiwa kuwa ni mambo yasiyokuwa ya kawaida kutoka kwa shaytwaan kwa lengo la kumpotosha yeye na kuwafanya wengine kupotea kupitia yeye. Msisahau kidhibiti hichi kilicho katika Qur-aan.

 

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-Furqaan (01) http://alfawzan.af.org.sa/node/2044
  • Imechapishwa: 06/10/2016