Tayammum kwa udongo, marumaru n.k.

Swali: Je, Hadiyth isemayo:

“… mpaka alipoelekea ukuta na akapangusa.”

Inafahamisha juu ya kufaa kufanya Tayammum kwa sehemu zinatokana na ardhi kama vile udongo, marumaru na kadhalika?

Jibu: Aina ya mchanga. Ni mamoja ni kutokana na ukuta au ardhi. Haja ikipelekea kitu kingine kama vile kile kilichoko ardhini au katika ardhi ya mchanga, basi atafanya Tayammum kutokana nayo:

فَاتَّقُوا اللَّـهَ مَا اسْتَطَعْتُمْ

”Mcheni Allaah muwezavyo.” (64:16)

Hilo ni kutokana na kuenea kwa Hadiyth na kuenea kwa Aayah:

فَلَمْ تَجِدُوا مَاءً فَتَيَمَّمُوا صَعِيدًا طَيِّبًا

“… na msipate maji, basi kusudieni [fanyeni Tayammum kwa] udongo ulio safi.”[1]

[1] 05:06

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/23567/هل-يجوز-التيمم-بالطين-والرخام-ونحوهما
  • Imechapishwa: 11/02/2024