Tawhiyd kwa mujibu wa Mu´attwilah

Wenye kuzikanusha sifa za Allaah wameingiza katika Tawhiyd-ur-Rubuubiyyah kupinga sifa. Mu´attwilah kwa tabaka na madhehebu yao mbali mbali wamesema kuwa maana ya Tawhiyd ni kukanusha sifa [za Allaah] na kusema ya kwamba kuthibitisha sifa kunalazimisha kupatikana kwa “walio wajibu” wengi. Aliye wajibu kwa mujibu wao ni Allaah kama jinsi viumbe wanawaita kuwa ni “awezekanaye”. Kutaka kulikimbia hilo ndio wakaenda kukanusha Sifa mpaka kusipatikane “walio wajibu” isipokuwa mmoja. Wanadai ya kwamba ikiwa watathibitisha kusikia, kuona, ujuzi na uwezo, basi walio wajibu watapatikana wengi. Hii ni batili kubwa kabisa. Ni uharibifu.

Hakupatikani kitu nje kwa kuthibitisha dhati peke yake pasi na sifa wala majina. Hakupatikani kitu nje isipokuwa kina jina na sifa. Tukikanusha sifa na majina kwa mtu basi hawezi kupatikana kwa hali yoyote. Kwa mfano ukisema kuna kitu kilichopo lakini hata hivyo sio kirefu, hakionekani, sio cha kina, hakiko juu, hakiko chini, hakiko nyuma, hakiko mbele, hakiko upande wa kulia na wala hakiko upande wa kushoto, kitu chenye sifa kama hizi ni kitu kisichopatikana duniani.

Watu hawa wamekanusha Allaah kuwa na majina na sifa. Hiyo ina maana ya kwamba hawakuthibitisha [kuwepo kwa] Mola wala Muumba kwa uhakika. Si jengine isipokuwa ni ndoto tu.

  • Mhusika: ´Allaamah ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah ar-Raajhiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-Hidaayah ar-Rabbaaniyyah fiy Sharh al-´Aqiydah at-Twahaawiyyah (01/35-36)
  • Imechapishwa: 07/06/2020