Imani ya Huluul na Wahdat-ul-Wujuud ndio ukafiri mkubwa kabisa

Watu hawa Jahmiyyah wamevuka mipaka na kusema ya kwamba Allaah Yuko kila mahali – Ametakasika kwa Allaah kwa yale wanayoyasema utakasikaji ulio mkubwa. Walipofikia katika imani ya kusema kuwa Allaah anapatikana kwenye kila kiumbe (Huluul) na kusema kuwa yuko kila mahali (Wahdat-ul-Wujuud) ndio hilo likawapelekea katika Tawhiyd hii – ambayo wao wanaita kuwa ni Tawhiyd ilihali ni aina kubwa kabisa ya Shirki – na kusema ya kwamba Fir´awn yuko katika usawa na alipatia pale aliposema:

أَنَا رَبُّكُمُ الْأَعْلَىٰ

“Mimi ni mola wenu mkuu.” (79:24)

Wakasema vilevile ya kwamba waabudu masanamu wako katika haki na usawa kwa kuwa bado wanachokifanya wanamwabudu Allaah na hawamwabudu mwingine. Wakasema pia ya kwamba hakuna tofauti katika uharamu baina ya mama, dada na mtu ajinabi, wala maji na pombe, wala baina ya uzinzi na ndoa. Wakasema yote hayo [uhakika wake] yanatokama na [uwepo wa] dhati moja.

  • Mhusika: ´Allaamah ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah ar-Raajhiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-Hidaayah ar-Rabbaaniyyah fiy Sharh al-´Aqiydah at-Twahaawiyyah (01/36)
  • Imechapishwa: 07/06/2020