Swali: Vipi anatubia mtu aliyetia chanjo mwilini mwake?

Jibu: Tawbah inafuta yaliyotangulia.

Swali: Vipi kwenda hospitalini kufuta chanjo hii?

Jibu: Ni sawa ikiwa inawezekana. Hata hivyo hapana vibaya isipowezekana. Ikiwa ndugu zake ndio walimchanja basi dhambi zinawapata ndugu zao hao. Ikiwa yeye ndiye aliyejichanja katika hali ya ukubwa kisha akatubia, basi Allaah anamsamehe. Ni sawa akiweza kuiondoa bila kumdhuru. Vinginevyo anasamehewa. Tawbah inafuta yote yaliyotangulia. Ni sawa akiweza kuiondoa pasi na matatizo.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/24111/ماذا-يفعل-صاحب-الوشم-اذا-اراد-ان-يتوب
  • Imechapishwa: 31/08/2024