Swali: Je, ni lazima kutubia kutokana na madhambi madogo?

Jibu: Ndio, ni lazima kutubia kwa kila dhambi:

يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا تُوبُوا إِلَى اللَّـهِ تَوْبَةً نَّصُوحًا

“Enyi walioamini! Tubieni kwa Allaah tawbah ya kwelikweli.”[1]

َتُوبُوا إِلَى اللَّـهِ جَمِيعًا أَيُّهَ الْمُؤْمِنُونَ لَعَلَّكُمْ تُفْلِحُونَ

“Tubuni kwa Allaah nyote, enyi waumini, mpate kufaulu.”[2]

Amewasemeza waumini. Mtu hawi muumini kama hajiepushi na madhambi madogo. Anakuwa ni muumini mwenye imani pungufu.

Swali: Nikijiepusha na madhambi makubwa bado nalazimika kutubia kwa madhambi madogo?

Jibu: Ukijiepusha na madhambi madogo yanaondoka yale madhambi madogo. Hata hivyo mtu akitubia kwayo inakuwa kwa njia ya kupatiliza na kujihadhari. Kwani mtu hajui kama imani yake imesalimika na madhambi makubwa au yuko na sehemu yake. Kwa hiyo mtu daima yuko khatarini. Hakika usengenyi, umbea, ribaa, kukata udugu, kuwaasi wazazi, matusi na mambo mengine yote yanaingia katika madhambi makubwa. Tunamuomba Allaah usalama. Ni nani ambaye amesalimika na kusenganya?

[1] 66:08

[2] 24:31

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/24320/هل-التوبة-من-الصغاىر-واجبة
  • Imechapishwa: 29/09/2024