Swali: Ni ipi tafsiri ya maneno Yake Allaah (Ta´ala):
مَن كَانَ يُرِيدُ الْحَيَاةَ الدُّنْيَا وَزِينَتَهَا نُوَفِّ إِلَيْهِمْ أَعْمَالَهُمْ فِيهَا وَهُمْ فِيهَا لَا يُبْخَسُونَ أُولَـٰئِكَ الَّذِينَ لَيْسَ لَهُمْ فِي الْآخِرَةِ إِلَّا النَّارُ
”Anayetaka maisha ya dunia na mapambo yake Tutawalipa kikamilifu matendo yao humo, nao humo hawatopunjwa. Hao ndio wale ambao hawatokuwa na chochote katika Aakhirah isipokuwa Moto…”[1]?
Jibu: Aayah hii inawahusu makafiri. Kinachotambulika kwa wanazuoni ni kwamba inawahusu makafiri. Kuna maoni pia yanayosema kuwa inawajumuisha wale wanaojionyesha kwa matendo yao. Matendo yao yanaharibika. Hata hivyo kinachotambulika ni kwamba imeshuka juu ya makafiri. Lakini ujumla wake ni wajibu kujihadhari, kwa sababu amesema:
وَحَبِطَ مَا صَنَعُواْ فِيهَا وَبَاطِلٌ مَّا كَانُواْ يَعْمَلُونَ
”… yataharibika yale yote waliyoyafanya humo [hapa duniani] na yatabatilika yale waliyokuwa wakiyatenda.”
Haya hayawahusu wengine isipokuwa makafiri tu:
وَلَوْ أَشْرَكُوا لَحَبِطَ عَنْهُم مَّا كَانُوا يَعْمَلُونَ
“Lau wangemshirikisha bila shaka yangeporomoka yale waliyokuwa wakitenda.”[2]
Lakini hata hivyo inaweza kumuhusu pia mwenye kujionyesha katika yale aliyojionyesha kwayo. Yale aliyojionyesha kwayo yanaharibika. Tunamuomba Allaah usalama.
[1] 16:15
[2] 06:88
- Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
- Mfasiri: Firqatunnajia.com
- Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/24327/تفسير-من-كان-يريد-الحياة-الدنيا-وزينتها
- Imechapishwa: 29/09/2024
Swali: Ni ipi tafsiri ya maneno Yake Allaah (Ta´ala):
مَن كَانَ يُرِيدُ الْحَيَاةَ الدُّنْيَا وَزِينَتَهَا نُوَفِّ إِلَيْهِمْ أَعْمَالَهُمْ فِيهَا وَهُمْ فِيهَا لَا يُبْخَسُونَ أُولَـٰئِكَ الَّذِينَ لَيْسَ لَهُمْ فِي الْآخِرَةِ إِلَّا النَّارُ
”Anayetaka maisha ya dunia na mapambo yake Tutawalipa kikamilifu matendo yao humo, nao humo hawatopunjwa. Hao ndio wale ambao hawatokuwa na chochote katika Aakhirah isipokuwa Moto…”[1]?
Jibu: Aayah hii inawahusu makafiri. Kinachotambulika kwa wanazuoni ni kwamba inawahusu makafiri. Kuna maoni pia yanayosema kuwa inawajumuisha wale wanaojionyesha kwa matendo yao. Matendo yao yanaharibika. Hata hivyo kinachotambulika ni kwamba imeshuka juu ya makafiri. Lakini ujumla wake ni wajibu kujihadhari, kwa sababu amesema:
وَحَبِطَ مَا صَنَعُواْ فِيهَا وَبَاطِلٌ مَّا كَانُواْ يَعْمَلُونَ
”… yataharibika yale yote waliyoyafanya humo [hapa duniani] na yatabatilika yale waliyokuwa wakiyatenda.”
Haya hayawahusu wengine isipokuwa makafiri tu:
وَلَوْ أَشْرَكُوا لَحَبِطَ عَنْهُم مَّا كَانُوا يَعْمَلُونَ
“Lau wangemshirikisha bila shaka yangeporomoka yale waliyokuwa wakitenda.”[2]
Lakini hata hivyo inaweza kumuhusu pia mwenye kujionyesha katika yale aliyojionyesha kwayo. Yale aliyojionyesha kwayo yanaharibika. Tunamuomba Allaah usalama.
[1] 16:15
[2] 06:88
Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
Mfasiri: Firqatunnajia.com
Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/24327/تفسير-من-كان-يريد-الحياة-الدنيا-وزينتها
Imechapishwa: 29/09/2024
https://firqatunnajia.com/matendo-ya-wenye-kujionyesha/
Mshirikishe mwenzako:
- Click to share on Telegram (Opens in new window)
- Click to share on WhatsApp (Opens in new window)
- Click to print (Opens in new window)
- Click to email a link to a friend (Opens in new window)
- Click to share on Facebook (Opens in new window)
- Click to share on Twitter (Opens in new window)
- Click to share on Pocket (Opens in new window)