Swali: Baadhi ya wanachuoni wanasema Tawassul ni suala la ki-Fiqh na sio la ki-´Aqiydah. Vipi kuhusu hilo?

Jibu: Kufanya Tawassul katika du´aa kwa jaha ya Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam), dhati yake au manzilah yake ni kitu hakikuwekwa katika Shari´ah. Ni njia inayopelekea katika shirki. Utafiti katika suala hili ili kubainisha haki [imetubainikia kuwa] ni suala la ki-´Aqiydah.

Kuhusu kufanya Tawassul kwa Allaah kwa majina Yake, sifa Zake, kwa kumfuata Mtume na kwa matendo juu ya ´Aqiydah na hukumu alizokuja nazo ni jambo lililowekwa katika Shari´ah.

  • Mhusika: al-Lajnah ad-Daaimah
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Fataawaa al-Lajnah ad-Daaimah (1/347)
  • Imechapishwa: 24/08/2020