Mtume Muhammad ameumbwa kutoka kwenye nuru ya Allaah?

Swali: Nimemsikia mwalimu mwenye kusema kuwa Muhammad (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) ameumbwa kutoka kwenye nuru ya Allaah. Je, hili ni sahihi?

Jibu: Maoni ya mwalimu huyu ni ya makosa. Inaenda kinyume na dalili za Qur-aan na Sunnah. Hakika dalili, hisia na yenye kushuhudiwa vyote vinajulisha kuwa ameumbwa kutokana na baba na mama ambao ni ´Abdullaah bin ´Abdil-Muttwalib na Aaminah bint Wahb. Ukoo wake ni wenye kujulikana.

  • Mhusika: al-Lajnah ad-Daaimah
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Fataawaa al-Lajnah ad-Daaimah (1/309)
  • Imechapishwa: 24/08/2020