Tawassul kwa matendo na utume wa Muhammad

Swali: Je, inajuzu kufanya Tawassul kwa matendo ya Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) na utume wake?

Jibu: Hapana. Usifanye Tawassul kwa Allaah kwa matendo ya mtu mwingine. Tawassul kwa Allaah kwa matendo yako mema. Ama kuhusu matendo ya mwingine ni ya kwake na wewe huna ushirikiano wowote. Kila mmoja ana matendo yake:

تِلْكَ أُمَّةٌ قَدْ خَلَتْ ۖ لَهَا مَا كَسَبَتْ وَلَكُم مَّا كَسَبْتُمْ ۖ وَلَا تُسْأَلُونَ عَمَّا كَانُوا يَعْمَلُونَ

“Huo ni ummah kwa umeshapita, utapata uliyoyachuma nanyi mtapata mliyoyachuma na wala hamtoulizwa juu ya yale waliyokuwa wakiyatenda.” (02:141)

Usitawassul kwa Allaah kwa matendo ya mtu mwingine. Tawassul inakuwa kwa matendo mema ya mtu mwenyewe.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Qaa´idah Jaliylah fiyt-Tawassul wal-Wasiylah (34) http://alfawzan.af.org.sa/node/2131
  • Imechapishwa: 13/07/2020