Kuomba kwa mapenzi ya Allaah kwa Muhammad

Swali: Inajuzu kwa mtu kuomba du´aa kwa kusema:

“Ee Allaah! Mimi nakuomba kwa kumpenda Kwako Muhammad (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam)?”

Jibu: Hapana, asiombe hivo ya kwamba anamuomba kwa kumpenda Kwake Muhammad (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam). Hili halina uhusiano wowote na mwombaji. Badala yake aombe kwa kusema:

“Ee Allaah! Nakuomba kwa kumpenda kwangu Mtume Wako (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam).”

Hichi ndio kitendo chako. Kumpenda kwako Mtume wa Allaah au kumpenda kwako Allaah ni kitendo chako ambacho unatawassul kwacho kwa Allaah. Ama kuomba kwa matendo ya wengine haifai.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Qaa´idah Jaliylah fiyt-Tawassul wal-Wasiylah (32) http://alfawzan.af.org.sa/node/2144
  • Imechapishwa: 13/07/2020