Haijuzu kusikiliza kanda na kaseti kama hizi

Swali: Ni kitu kinachoingia katika kanuni hii kusikiliza kanda ilio na visa vya mawaidha na mambo yenye kwenda kinyume na watu wakaongoka kwa sababu ya kuisikiliza. Je, kanda kama hii ikemewe?

Jibu: Hili halijuzu. Kanda inatakiwa iwe imesafishwa na uongo, shirki na Bid´ah. Kanda inatakiwa iwe ni yenye kuafikiana na maneno ya Allaah na Mtume Wake na maneno ya wanachuoni wahakiki. Ama kuhusu kanda iliochanganya kati ya haki na batili haijuzu kuisikiliza.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Qaa´idah Jaliylah fiyt-Tawassul wal-Wasiylah (32) http://alfawzan.af.org.sa/node/2144
  • Imechapishwa: 13/07/2020