Tarjama za Qur-aan nyingi leo zina makosa tele

Swali: Ambaye ana upeo wa kufanya tarjama ya maana ya Qur-aan Tukufu. Pale ambapo Aayah moja itakuwa na maana zaidi ya moja na wafasiri wa Qur-aan wakatofautiana katika kuifasiri, mwenye kufanya tarjama atachagua maoni yepi katika kufasiri Aayah hiyo?

Jibu: Enyi ndugu! Tarjama haina maana ya mtu aende kufasiri Qur-aan. Mwenye kufanya tarjama anachotakiwa ni kuleta kitabu miongoni mwa vitabu vya Tafsiyr kinachoaminiwa – iwe ni kitabu kinachoaminiwa – ndio atarjumu [kupitia kitabu hicho]. Asitarjumu kwa mujibu wake. Haifai kwake kutarjumu kwa mujibu wake. Anachotakiwa ni kutarjumu kwa kupitia Tafsiyr miongoni mwa Tafsiyr zenye kuaminika. Kwa ajili hii ndio maana inaitwa “Tarjama ya maana ya Qur-aan Tukufu” na sio tarjama ya Qur-aan. Hakuna anayejua tarjama ya maana ya Qur-aan Tukufu isipokuwa wafasiri wahakiki. Ama mtarjumu yeye huwa ni mwenye kunukuu tu kutoka kwenye lugha na kwenda lugha nyingie. Hivyo basi, asitarjumu na kufasiri kwa mujibu wake.

Kumepatikana makosa mengi kutoka kwa watu hawa katika kutarjumu kwao Qur-aan kwa sababu wameegemea ufahamu wao. Kumepatikana makosa mengi katika tarjumu kwa sababu hii.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: at-Tafsiyr al-Mufasswal (14) http://www.alfawzan.af.org.sa/sites/default/files/tf–1427-10-15.mp3
  • Imechapishwa: 19/08/2020