Swali: Mimi nafanya kazi kwenye dula la kuuza nguo. Mmiliki wa duka anapinga kuswali swalah ya Tarawiyh msikitini kwa hoja kwamba dula linafungwa muda wote huo nisipouza kitu katika kipindi chote hicho. Je, inafaa kuswali peke yangu nyumbani baada ya kumaliza kazi?

Jibu: Swalah ya usiku imefanyiwa wasaa. Aiswali nyumbani au pamoja na wengine. Ikiwa muda wa kazi ni katika wakati wa Tarawiyh basi unalazimika kufanya kazi katika wakati wa Tarawiyh. Kwani unapokea malipo juu ya hilo na Tarawiyh ni kitu cha kujitolea. Kwa hivyo ni lazima kwako kutekeleza mkataba kati yako wewe na bosi wako. Ikiwa mkataba wa kazi unakutaka uanze kazi moja kwa moja baada ya swalah ya faradhi, swalah ya ´Ishaa, basi unapaswa kuanza kazi yako. Isipokuwa kwa idhini yake akikuruhusu. Unaweza vilevile kuswali Tahajjud usiku nyumbani kwako.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/9784/حكم-صلاة-التراويح-في-المنزل
  • Imechapishwa: 05/04/2023