Talaka ya anayedai kuwa amefanyiwa uchawi

Swali: Ni ipi hukumu ya Talaka ya aliyefanyiwa uchawi?

Jibu: Talaka inapita. Akitaliki Talaka inapita. Baadhi ya watu wanakuwa na haraka na kusema kwamba wamefanyiwa uchawi ilihali hana uhakika wa uchawi. Maadamu akili zake bado ziko na yeye, ana akili, Talaka inapita. Ama ikithibiti kweli ya kwamba akili yake imabadilika, kama mfano wa mwendawazimu, Talaka yake haipiti. Mwendawazimu Talaka yake haithibiti. Ama kudai kuwa ana uchawi na yeye ana akili, anauza na kununua na bado akili yake iko pamoja naye, madai haya ni batili hayakubaliwi.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: http://subulsalam.com/play.php?catsmktba=14579
  • Imechapishwa: 05/05/2015