Ibn Baaz kuhusu kuzungumza na jini wakati wa haja

Swali: Baadhi ya watu wanazungumza na jini na wanachukua ahadi kutoka kwake na mfano wa hayo na wanawauliza baadhi ya maswali. Ni ipi hukumu ya hilo?

Jibu: Ikiwa inahusiana na sababu ya kulitoa, ikiwa anazungumza nalo kwa ajili ya kutaka ahadi kutoka kwake, kulitahadharisha na kubainisha sababu [sauti haisikiki] kitu hiki, ikiwa ni kuhusiana na hili hakuna neno. Makusudio ni kwamba mtu afanye mambo ambayo atafikia kulitoa.

Swali: Na ni ipi hukumu ya kuchukua ahadi kutoka kwa jini?

Jibu: Ikiwa anataka kuchukua ahadi kwake asirudi [sauti haisikiki] na atahadhari na hilo, hakuna neno.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: http://subulsalam.com/play.php?catsmktba=14579
  • Imechapishwa: 05/05/2015