Swali: Je, inajuzu kwa mtu kutaka msaada kutoka kwa jini Muislamu ili amsaidie kutoa uchawi au amuoneshe mahala ulipo uchawi kwa njia ya kufanya sababu na sio kwa njia ya kuwaomba msaada badala ya Allaah?

Jibu: Haijuzu kuwaomba msaada majini wala kuwauliza. Ni wajibu kutahadhari hilo. Hata hivyo ananasihiwa. Ni wajibu kwake (msomeaji) amnasihi kumcha Allaah, asiwaudhi watu, asiwafanyie uadui watu ikiwa anamuamini Allaah na siku ya Mwisho, ´Ibaadah inamuwajibikia juu yake na ataulizwa. Ni wajibu kunasihiwa na kutahadharishwa kuwafanyia watu uadui na kuwaudhi.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: http://subulsalam.com/play.php?catsmktba=14579
  • Imechapishwa: 05/05/2015