Takbiyr kila wakati wa kusujudu na wakati wa kuinuka

Swali: Baadhi ya imamu wanapoinuka kutoka katika Takbiyr ya kisomo wanaleta Takbiyr na wengine huanza moja kwa moja kwa kusoma bila ya kuleta Takbiyr.

Jibu: Hapana, Sunnah ni kuleta Takbiyr akiwa ndani ya swalah. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alikuwa akipiga Takbiyr wakati wa kila kuinuka na wakati wa kila kuinama. Akisujudu kwa ajili ya kisomo ndani ya swalah ni kama Sujuud ya swalah na hivyo anatakiwa kuleta Takbiyr wakati wa kusujudu na pia alete Takbiyr wakati wa kuinuka akiwa ndani ya swalah.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/23762/هل-يكبرللرفع-من-سجدة-التلاوة-في-الصلاة
  • Imechapishwa: 24/04/2024