Swali: Je, Qunuut inamuhusu pia anayeswali peke yake na mwanamke anayeswali peke yake?

Jibu: Wakati wa majanga. Waislamu wanapofikwa na maafa basi anatakiwa kuleta Qunuut na kumwomba Allaah ainusuru dini Yake na kwamba Allaah awatosheleza na shari ya maadui. Hivo ndivo Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alikuwa akifanya. Mara nyingi ilikuwa ni katika Fajr, wakati mwingine akifanya (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) hivo Maghrib na nyakati nyenginezo. Hii inaitwa Qunuut ya majanga.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/23768/هل-يشرع-قنوت-النوازل-للمنفرد
  • Imechapishwa: 24/04/2024