Swali: Ni lini zinaanza na kumalizika Takbiyr katika ´Iyd-ul-Fitwr na ´Iyd-ul-Adhwhaa?
Jibu: Kuhusu katika ´Iyd-ul-Fitwr, zinaanza pale ambapo watu wanapotoka kwenda kuswali. Zinaendelea kabla ya swalah. Hata hivyo hapana vibaya watu wakaleta Takbiyr katika ile siku nzima ya ´iyd.
Kuhusu ´Iyd-ul-Adhwaa, Takbiyr zinasomwa katika yale masiku ya Tashriyq. Hata hivyo isifanywe ni jambo maalum zikasomwa baada ya swalah. Pia hapana vibaya kila mmoja akaleta Takbiyr peke yake. Au mmoja akaleta Takbiyr na wengine wakamfuata au wakaleta Takbiyr kwa pamoja. Hata hivyo salama zaidi ni kila mmoja alete Takbiyr peke yake. Haikupokelewa kuwa walikuwa wakileta Takbiyr kwa sauti ya pamoja. Isitoshe Takbiyr hii inatakiwa kukaririwa kusikokuwa chini ya mara tatu. Hata hivyo hapana vibaya endapo wataleta zaidi ya hivyo.
- Muhusika: ´Allaamah Muqbil bin Haadiy al-Waadi´iy
- Tarjama: Firqatunnajia.com
- Marejeo: Qam´-ul-Mu´aanid, uk. 366
- Imechapishwa: 05/06/2025
Mshirikishe mwenzako:
- Click to share on Telegram (Opens in new window) Telegram
- Click to share on WhatsApp (Opens in new window) WhatsApp
- Click to print (Opens in new window) Print
- Click to email a link to a friend (Opens in new window) Email
- Click to share on Facebook (Opens in new window) Facebook
- Click to share on X (Opens in new window) X
- Click to share on Pocket (Opens in new window) Pocket