Tajiri hataki kuhiji kwa kisingizio cha madeni

Swali 64: Baadhi ya watu ana zaidi ya miaka 50 na wana mali, mashamba, ardhi na nyumba, na ana deni, lakini hajatekeleza faradhi ya Hijjah. Akinasihiwa ahiji hujitetea kwa deni, pamoja na kuwa ana uwezo wa kulilipa deni lake kwa kuuza baadhi ya mali zake. Je, inafaa kwake kuweka dhamana ya deni kwa rehani kisha ahiji au hilo deni ni udhuru kwake?

Jibu: Ninaona kwamba auze katika mali hizi ambazo hazihitajii kisha alipe deni lake na ahiji, kwa sababu mtu huyu ni tajiri. Utajiri si wingi wa pesa taslimu, bali utajiri ni wingi wa mali zinazozidi mahitaji ya mtu. Ikiwa ana majengo mengi anaweza kuuza moja katika kumi yake kisha ahiji. Ni wajibu kwake kuuza na ahiji. Huu ndio wajibu wake. Mtu huyu hajui huenda akaamka asifikie jioni au akaingia jioni asifikie asubuhi. Hivyo mali hizi zitabaki kwa watu wengine wakizineemeka nazo na yeye atabeba madhara yake.

  • Muhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Majmuu´-ul-Fataawaa (21/67-68)
  • Imechapishwa: 08/05/2026