Inafaa kwangu kuchelewesha Hajj?

Swali 59: Umri wangu ni miaka 30. Je, inajuzu kwangu kuichelewesha Hajj hadi mwaka ujao, hali ya kuwa nina uwezo wa kuhiji sasa?

Jibu: Haijuzu. Mwenye kuwajibikiwa Hajj, basi inamlazimu kuharakisha kuitekeleza. Kwa sababu mtu hajui kitakachomtokea. Huenda akapoteza mali hii, huenda akaugua katika siku zijazo au huenda akafa. Mwenye kuwajibikiwa Hajj, basi inamlazimu kuharakisha kuitekeleza na haifia kwake kuichelewesha.

  • Muhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Majmuu´-ul-Fataawaa (21/64-65)
  • Imechapishwa: 08/05/2026