Mwanamke amepata taarifa ya kifo cha mumewe akiwa katika Hajj

Swali 50: Ikiwa mwanamke ametoka kwenda kufanya Hajj na baada ya kufika Jeddah akasikia kifo cha mume wake. Je, aendelee kukamilisha Hajj au akae eda ya kufiwa?

Jibu: Anakamilisha Hajj. Kwa sababu ikiwa atarudi, basi atarudi kwa safari, na ikiwa atabaki, atabaki katika safari inayoendelea. Kwa hivyo anakamilisha Hajj, khaswa ikiwa ni Hajj faradhi. Kisha baadaye anarudi. Hata ikiwa ni ya Hajj ya kujitolea, anaikamilisha.

  • Muhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Majmuu´-ul-Fataawaa (21/58)
  • Imechapishwa: 08/05/2026