Nibaki namlea mtoto au nende kuhiji?

Swali 56: Mke wangu hajatekeleza faradhi ya Hajj mpaka sasa. Tuna mtoto wa miezi minne ambaye ananyonya kutoka kwa mama yake. Je, ahiji au abaki kwa mtoto wake?

Jibu: Ikiwa mtoto hataathirika wala hatadhurika kwa safari yake, kwa kuwa ananyonya maziwa yasiyo ya mama yake na yupo anayemlea ulezi kamili, basi hakuna ubaya juu yake kuhiji, khaswa ikiwa ni Hajj ni faradhi. Ama ikiwa kunakhofiwa juu ya mtoto, basi si halali kwake kuhiji, hata kama Hajj ni faradhi. Kwa sababu mwanamke anayenyonyesha anaruhusiwa kuacha kufunga faradhi ikiwa anakhofia juu ya mtoto wake, basi vipi asiache kuharakisha Hajj ikiwa anachelea juu ya mtoto wake? Ikiwa anachelea juu ya mtoto, basi wajibu ni abaki. Atakapokua mkubwa mwaka ujao, basi atahiji. Hakuna ubaya juu yake ikiwa atabaki na akaacha Hajj, kwa sababu Hajj katika hali hii haimlazimu kuharakisha.

  • Muhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Majmuu´-ul-Fataawaa (21/62-63)
  • Imechapishwa: 08/05/2026