Swali: Je, inafaa kuswali Rak´ah mbili za mamkuzi ya msikiti na sisi tunaenda kuswali ´iyd msikitini au haifai kuswali Rak´ah mbili katika swalah ya ´iyd?

Jibu: Kiwanja cha kuswalia ´iyd hakina mamkuzi ya msikiti. Hakina hukumu moja kama misikiti. Hakina mamkuzi ya msikiti. Bali mtu anatakiwa kuketi chini. Isitoshe wakati huo mtu amekatazwa kuswali. Kiwanja cha kuswalia ´iyd sio msikiti. Lakini ikiwa swalah ya ´iyd inaswaliwa katika msikiti wa kawaida na uliozoeleka, wakiswali ´iyd kwenye misikiti basi kumesuniwa kuswali swalah ya mamkuzi ya msikiti ijapo ni katika wakati ambapo mtu amekatazwa kuswali kwa mujibu wa maoni sahihi. Amesema (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam):

“Anapoingia mmoja wenu msikiti basi asiketi chini mpaka kwanza aswali Rak´ah mbili.”

Wakati siku moja (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alipomwona  bwana mmoja ameketi chini alimwambia:

“Simama na uswali Rak´ah mbili.”

Kuhusu kiwanja cha kuswalia ´iyd kinachokuwa jangwani hakina hukumu moja kama msikiti. Kwa hivyo mtu akija na jua halijachomoza, basi ataketi chini. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alikuwa haswali swalah ya ´iyd si kabla wala baada yake.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/16566/مصلى-العيد-ليس-له-تحية
  • Imechapishwa: 29/04/2022